MALI ZA SINGIDA UNITED ZAPIGWA MNADA
Mali mbalimbali za timu ya Singida United zimepigwa mnada na Kampuni ya Udalali ya Majembe Auction Mart ili kulipa kodi ya pango iliyokuwa inadaiwa na Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Singida (NHC).
Afisa wa kampuni hiyo Godwin Binamu amesema wamefikia uamuzi wa kuuza mali hizo ikiwemo vitanda, magodoro, kompyuta na masofa baada ya uongozi wa timu hiyo kushindwa kulipa kodi ya pango ya zaidi ya shilingi milioni tatu licha ya kuongezewa muda wa kufanya malipo.
Wakati mali zake zikinunuliwa na wananchi mbalimbali wa mkoa wa Singida katika mnada huo, kikosi cha Singida United kiko Jijini Arusha kikijiandaa kwaajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Simba, katika mwendelezo wa ligi kuu Tanzania Bara.
CHANZO: AZAM TV








Kuendesha timu ni gharama kubwa....lazima watu wajue
ReplyDeleteYaani timu ya daraja la kwanza inashindwa kulipa tshs.3m.Iko kazi kubwa
ReplyDeletehv hyo timu haina uongoz hadi wanashindwa na kodi?
ReplyDelete