MARCUS Rashford leo ameonyesha umwamba wake Kwa kufunga bonge moja ya bao mbele ya Liverpool kwenye mchezo wa tisa wa Ligi Kuu England.
Rashford alipachika bao hilo dakika ya 36 na kumuacha kwenye mataa mlinda mlango Allison na kuwafanya Liverpool waishiwe nguvu kipindi cha kwanza Uwanja wa Old Trafford.
Sadio Mane alipachika bao la kusawazisha dakika ya 43 teknolojia ya VAR ilikataa bao hilo kwa kuwa uligusa mkono kabla ya kuzama wavuni.
Iliwabidi Liverpool isubiri mpaka dakika ya 85 walipopachika bao kupitia Adam Laliana na kuweka mzani Sawa.
Mchezo ulikuwa ni wa ubabe kwani kila mchezaji alikuwa bondia.
Liverpool inasalia kileleni ikiwa na pointi 25 huku Manchester United ikiwa nafasi ya 10 na pointi zake 10.








0 COMMENTS:
Post a Comment