MANCHESTER United na Chelsea zimewafungia baadhi ya mashabiki wao maisha kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo udhalilishaji.
Miongoni mwa sababu hizo pia ni ubaguzi wa rangi na uvunjifu wa amani na klabu hizo zimekemea vilivyo tabia hizo.
Manchester United imemfungia shabiki wake ambaye alionyesha viashiria vya ubaguzi wa rangi dhidi ya staa wa Liverpool, Trent Alexander-Arnold Jumapili iliyopita.
Taarifa ya klabu inasema kwamba :" Ubaguzi wa rangi na viashiria vyake havikubaliki kabisa, huyu shabiki hataruhusiwa kuingia tena Old Trafford,".
Chelsea nayo imewafungia wachezaji watatu kutokana na kitendo hicho cha ubaguzi wa rangi na imekemea tabia hiyo.








0 COMMENTS:
Post a Comment