October 27, 2019


MOHAMED Salah mshambuliaji wa Liverpool aliumia kifundo cha mguu wakati timu yake ilipokuwa ikicheza na Leicester City kwenye mchezo wa Ligi Kuu England wiki mbili zilizopita.

Alikosa mchezo wa kibabe dhidi ya Manchester United uliokamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Kwa sasa yupo fiti alicheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mbele ya nahodha wa Genk Mbwana Samatta.


Liverpool ilishinda mabao 4-1 mchezo huo na kusepa jumla na pointi tatu wakiwa nafasi ya pili wana jumla ya pointi sita.

Kwenye Ligi Kuu England Salah amefunga jumla ya mabao manne akitoa asisti tatu kwenye dakika 707 ambazo amecheza mpaka sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic