MZEE AKILIMALI ACHAFUA HALI YA HEWA YANGA
Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, mzee Ibrahim Akilimali ameibuka na kusema kuwa haoni dalili za Yanga ikiitoa Pyramids ya Misri katika mchezo wa mtoano wa Kombe la Shirikisho Afrika kutokana na uongozi wa timu hiyo kugoma kuwapa timu wazee kuishughulikia.
Mzee Akilimali ametoa kauli hiyo kufuatia Yanga kupangwa na timu hiyo katika hatua ya mtoano ambapo inatarajia kucheza mchezo wa kwanza Oktoba 27, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kabla ya kuelekea nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano.
Mzee Akilimali alisema kuwa wazee wa timu hiyo wamekuwa wakiiomba kwa ajili ya kuiweka sawa kabla ya kucheza na Waarabu hao wa Misri lakini wamekuwa wakipigwa chenga na uongozi wa timu hiyo bila kuwapa majibu ya maana.
“Niwe mkweli kwamba sioni dalili za Yanga ikiwaondoa Waarabu hasa kwa timu ambayo tupo nayo kwa sababu ukiangalia wachezaji wetu wote wamefungwa hawana uwezo wa kushindana kabisa, wanahitaji kufunguliwa lakini uongozi bado unatuwekea ngumu kila tunavyowaambia.
“Sisi tunataka watu ili tufanye mambo yetu na tuweze kufuzu makundi lakini wao hawana mpango wowote wa kutupa zaidi ya kutukimbia, wamepeleka mechi Mwanza lakini haiwezi kusaidia chochote maana kama unasajili wachezaji halafu kwao bado wanagombea tuzo kubwa ila hapa wanaonekana weupe, ndiyo wajue kama wamefungwa,” alisema mzee Akilimali.
Kama Saleh Ally kuna mahala unakwama.Ni haki ya kila mtu kusikilizwa na habari zake kutangazwa lakini kuna nyakati tutumie weledi kujua habari za kujenga na kuupeleka mpira mbele.Naona kila baada ya siku unakuwa na mahojiano na huyu Mzee na sijaona mchango chanya zaidi ya vitisho,kulialia na kujimwambafai kwako ambavyo havina msaada Kwa Yanga katika dhama hizi.Vinginevyo nitaanza amini kuwa Una agenda yako nyuma ya pazia.
ReplyDeleteHuyu n mmoja kati ya waandishi wanafiki anayetumika na asiyekuwa na weledi,uwa najiuliza kila Mara kwanini apewe nafasi kubwa mzee Akilimali katika magazine yake anayoongoza wakati siyo kiongozi kikatiba mbona awatumi waandishi wake kumhoji kila Mara mzee Kilomoni au Nkwabi kuhusiana na uozo wa Simba,tunaamini ameshikwa na tajiri wa Simba kwani imejidhihirisha hata ktk makala zake amekuwa mstari wa mbele kuitetea Simba inapoibuka zengwe ana tabia za kike kwani amekuwa akiandika mipasho dhidi ya waandishi wenzie ajirekebishe
ReplyDeleteHeee Simba inahusika vipi?.... hizo pumba zako mpelekee mzee Aklimali mkajadiliane jinsi ya kupungunza magoli ya Praymid
DeleteSimba inahusika nini hapo?Tatueni matatizo yenu wacheni kuitumia Simba kama scapegoat.
ReplyDeleteHii habari ni ya kibwege sana hasa kuelekea mchezo muhimu wa Yanga. Hii inalenga zaidi kuwagawa wana Yanga!!! Weledi wa uandishi wa habari ni pamoja na kubalance story, je umejaribu kuwasiliana na viongozi wa Yanga kuhusu hili!? Halafu kila siku nyie habari zenu source ni Akilimali , Insta page ya Manara hivi ndio mmeshindwa kujiongeza kabisa!!??
ReplyDeleteNyi waandishi huwa mnajidai kutoa maoni yenu kwa viongozi wa soka lakini kwa uandishi huu inaonesha wazi kuwa HAMJAIVA katika sekta hii muhimu ya habari... Kilichobakia ni kuto wa follow tu!!
Wapelekeni wachezaji wakafunguliwe.Acheni ubishi.Wapuuzi FC eti wachezaji wamefungwa?Ujinga hauna mipaka!!!
ReplyDeleteUkweli ni ujinga usio na mpaka.Acheni upuuzi concetrate na mechi yenu na Pyramids
Delete