ISSA Nampepeche bondia wa ngumi za kulipwa amefanikiwa kumchapa Ally Hamisi wa Moro kwa pointi katika pambano la usiku wa mabingwa lilofanyika usiku wa kuamika leo kwenye Ukumbi wa Club 361, Dar.
Pambano hilo lilikuwa na upinzani mkali kwa mabondia hao ila Nampepeche alionekana bora kutokana na kupiga ngumi nyingi za uhakika katika raundi zote sita kabla ya kutangazwa mshindi na majaji.
Baada ya ushindi huo, Nampepeche alitamba kuwa suala la kushinda kwake lilikuwa lipo wazi kutokana na kufanya maandalizi makali kabla ya pambano hilo huku akimtaka mpinzani wake akubali kushindwa.
Kwa upande wa Ally Hamisi akiri kuwa yeye ni bondia mdogo kutokana na rekodi ya mampano yake huku akiamini kwamba hajapigwa kutokana na madai ya mpinzani wake kutumia muda mwingi kurusha makofi badala ya ngumi kwenye pambano hilo huku yakiwa chini ya udhamini wa Gazeti la Championi, +255 Global radio, Smart Gin, Glady Matata na Kiwango Security.
Katika mapambano mengi, Maganga Kulwa amefanikiwa kumtwang ‘vitasa’ vya maana mpinzani wake Said Sudi na kupelekea kushinda kwa pointi pambano ambalo lilikuwa la raundi nne.
Bondia Abdallah Kingolwira kutoka Morogoro amefanikiwa kushinda kwa pointi katika pambano la raundi nne dhidi ya Ahmed Pelembela wa Dar aliyechukua nafasi ya Ibrahim Makubi aliyeshindwa kupanda ulingoni kutokana na kuumwa meno yaliyokuwa yamevimbisha mdomo.
Pia bondia Salum Omari amefanikiwa kumchapa kwa pointi William Joseph katika pambano la utangulizi ambalo lilikuwa la raundi nne.
0 COMMENTS:
Post a Comment