PATRICK AUSSEMS KUONDOKA SIMBA
INAELEZWA kuwa uongozi wa Klabu ya Nkana ya nchini Zambia, umepanga kumpa mkataba Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems kufuatia kuwepo kwa mchakato wa kuachana na kocha wao, Besto Chambesh.
Nkana wameanza mchakato huo kutokana na kocha wao kupewa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 23 itakayokwenda kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) itakayofanyika mwezi ujao nchini Misri.
Inadaiwa kamati ya ufundi ya timu hiyo, mpaka sasa imeshapendekeza majina ya makocha watatu ambao ni Aussems, Perry Mutapa wa Forest Rangers ya Zambia na CK Akounor aliyekuwa kocha wa Asante Kotoko ya Ghana.
Taarifa za uhakika kutoka nchini Zambia zinafafanua kuwa Mbelgiji huyo ni miongoni mwa majina ya makocha watatu wanaotajwa kupewa nafasi ya kocha kutokana na rekodi yake ya msimu uliopita katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
“Huku Zambia hizo taarifa za Nkana kumtaka kocha wa Simba zipo kwa sababu ni miongoni mwa makocha watatu ambao wanawatupia jicho kali kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Chambeshi ambaye atakuwa Misri na timu ya taifa ya vijana kama kocha mkuu.
“Shida ni kwamba wenyewe wameamua kufanya jambo la siri, kwa kuwa bado lipo kwenye idara ya ufundi ambayo inatakiwa kumaliza mchakato lakini ukiangalia kwa upande wa kocha wa Simba, anapewa nafasi kubwa kutokana na rekodi yake CAF msimu uliopita,” kilisema chanzo kutoka nchini humo.
Championi Jumatatu lilimtafuta Mtendaji Mkuu wa Nkana, Charles Chakatazya ambaye alisema kuwa: “Bado tupo na Besto, hatuwezi kusema nani atakuja kwa sasa kwa kuwa hakuna kilichokamilika na hayo ni maneno kila mmoja anaongea lake lakini kwa sasa sisi tunaangalia zaidi timu na mwalimu ambaye yupo.”
CHANZO: CHAMPIONI








Bado tunamuhitaj Aussem
ReplyDeleteHatuwez kuwapa kocha wetu,bad tunamuhitaj sn prof.Aussems
ReplyDelete