KAMPUNI ya kubashiri matokeo ya Premier Bet Tanzania imemtambulisha mshindi Andrea Sebastian mkazi wa wilayani Igunga, Tabora aliyejishindia zaidi ya Shilingi Milioni 53,636,841.
Mshindi huyo ameshinda baada ya kucheza mchezo wa kubashiri soka maarufu kwa jina la Sports Betting (SB) katika tawi lao la Igunga Oktoba 18, mwaka huu baada ya kuchagua timu 38 kwa dau la Shilingi 1,000.
Mkurugenzi Mkuu wa Premier Tanzania, Sami Matar amesema wanampongeza Sebastian kwa ushindi huo alioupata akiamini utabadilishi yake.
“Tunayo furaha kubwa kumkabidhi hundi mshindi wetu na tunajivunia kusema kuwa Premier Bet ni kampuni inayolipa pesa kwa haraka zaidi washindi wetu na tunamtaka Sebastian kuendelea kuwa mwenye bahati maishani mwake kote,”amesema Matar.
Kwa upande wa Sebastian amesema kuwa “Ninafuraha sana kushinda fedha hizi nyingi zitakazoenda kubadilisha maisha yangu.
“Nilikuwa na shauku kubwa sana baada ya kuanza kufuatilia matokeo ya mechi moja baada ya nyingine, baada ya kugundua kuwa kubashiri sahihi matokeo ya mechi zote 38 ninajiona ni mtu mwenye furaha dunia nzima," amesema.








0 COMMENTS:
Post a Comment