PYRAMIDS WAPEWA URAHISI NA YANGA
Kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga dhidi ya Pyramids FC kutoka Misri, kukosekana kwa David Molinga 'Falcao' na Moustafa Suleiman kunaweza kukawa kumewasaidia wapinzani hao.
Yanga itawakosa wachezaji hao wawili ambao wamekuwa wakipigiwa upatu mkubwa kuwa sehemu ya kikosi dhidi ya waarabu lakini hawatakuwepo sababu ya kukosa vibali.
Molinga na Mustafa hawajacheza tangu kuanza kwa mashindano ya kimataifa hivyo kukosekana kwao kunaweza kukawa faida kwa namna moja ama nyingine kwa Pyramids ambao wako nafasi ya tatu katika Ligi Kuu Misri.
Mashabiki wengi na baadhi ya wadau wa Yanga wamekuwa wakitamani kuwaona wawili hao wakiwa na kikosi cha timu hiyo katika mashindano ya kimataifa lakini imekuwa ngumu maana mpaka sasa hawajapata vibali.
Kuna uwezekano mkubwa Falcao na Moustafa wakawepo ndani ya kikosi cha Yanga baada endapo tu watatinga hatua ya makundi.








Viongozi wa yanga wawe wakweli kwa mashabiki wake , muda waliomsajiri molinga ulikuwa una faini na ukitoa nafadi ya kushiriki tu endapo timu itafuzu hatua ya makundi . sasa kudai caf inachelewesha kibali huu ni upotoshaji
ReplyDelete