October 16, 2019


Straika Mkongo wa Yanga, David Molinga ’Falcao’ ameweka ufalme wake ndani ya klabu hiyo kwa siku za karibuni kutokana na rekodi yake ya upachikaji mabao.

Molinga ambaye amesajiliwa msimu huu akitokea AC Rangers ya DR Congo tena kwa kuchelewa kwa sasa huenda akawa ndiyo mshambuliaji moto ndani ya klabu hiyo.

Kasi ambayo alianza nayo winga, Mnyarwanda Patrick Sibomana imeonekana kuzimika ghafla akiwa yeye amefunga mabao tisa lakini saba ya mechi za kirafiki na mawili mechi za kimataifa. Molinga katika mechi ambazo amecheza zile za kirafiki pamoja na za Ligi Kuu Bara amefunga jumla ya mabao saba mpaka sasa.

Straika huyo alifunga mabao hayo kwenye mechi za kirafiki dhidi ya Toto Africans (3-0), alifunga mawili, Friends Rangers (4-2) mawili, Pamba SC (1-1) bao 1 pamoja na mechi ya ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania sare ya 3-3 akifunga mabao mawili.

Staa huyo kwa mara ya kwanza Oktoba 27, mwaka huu ndipo ataweza kutumika kwenye mechi za kimataifa ile ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids kutoka Misri hii ni baada ya kuwa na vigezo tofauti na awali ambapo usajili wake ulichelewa. Ikumbukwe mpaka sasa kwenye Ligi Kuu Bara Yanga imefunga mabao manne katika mechi tatu na Molinga akifunga mawili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic