MEDDIE
Kagere, msh ambuliaji wa Simba ameendeleza moto wake wa kucheka na nyavu
baada ya kupachika bao lake la saba ndani ya ligi na kuipa pointi tatu timu ya
Simba mbele ya Azam FC.
Mchezo wa leo ambao umechezwa uwanja wa Taifa ulikuwa na ushindani mkubwa na ulitawaliwa
na ubabe mwingi kutokana na kila timu kuhitaji kupata pointi tatu.
Simba wakiwa
wenyeji wa mchezo iliwabidi wasubiri mpaka dakika ya 49 kuandika bao la
kuongoza lililopachikwa kimiani na Kagere akimalizia pasi ya Francis Kahata kwa
kichwa.
Ushindi huo
unaifanya Simba kuzidi kujikita kileleni ikiwa na pointi 15 na imecheza michezo
mitano kwa kusepa na pointi zote tatu.
Beki wa
Simba, Pascal Wawa ndiye alikuwa nyota wa mchezo kwani aliokoa hatari nyingi
kutoka kwa Chirwa ambaye alikuwa msubufu langoni akihaha kupata goli la ushindi
ila bahati haikuwa yao.
Simba
ilifanya mabadiliko kipindi cha pili kwa kumtoa Sharaf Shiboub nafasi yake
ikachukuliwa na Clatous Chama, Hassan Dilunga alimpisha Miraj Athuman, Francis
Kahata alimpisha Ibrahim Ajib kwa upande wa Azam FC alitoka Richard Djoud
aliyempisha Chilunda, Frank Domayo alimpisha Donald Ngoma.
Enter your comment...wanasimba tuendelee kushikamana mpaka kieleweke
ReplyDelete