October 27, 2019


Jeshi kamili la kikosi cha Simba sasa linakaribia kukamilika baada ya beki mwenye mapufu 'mithili ya mbwa' kutokana na pumzi kali ya kupanda na kushuka, Mohamed Hussein 'Tshambalala' pamoja straika anayesifika kwa kuwa na jicho la goli, John Bocco kurejea 'mdogomdogo'. 

Bocco amekuwa nje tangu Agosti 25, mwaka huu alipoumia wakati wa mechi ya raundi ya awali dhidi ya UD Songo ya Msumbiji iliyopigwa Uwanja wa Taifa na kumalizika kwa sare ya bao 1-1, akiungana na Tshabalala aliyeumia hivi karibuni akiwa katika majukumu na timu ya Taifa, Taifa
Stars.

Jana wachezaji hao ambao wamekuwa chachu ya ushindi katika kikosi cha Stars, walikuwa wakifanya mazoezi mepesi pamoja na kocha wa viungo wa timu hiyo wakati wachezaji wenzao wakiendelea kujifua kwa nguvu kwenye mazoezi yalikuwa yakiendelea viwanja vya Gymkhana.

"John Bocco na Mohamed Hussein wanaendelea na mazoezi mepesi. Hivi karibuni watakuwa wamepona na kuendelea kuwapa burudani Wanasimba," ilieleza taarifa ya Simba.

Simba iliyopo kileleni mwa Ligi Kuu Bara baada ya kushinda mechi zake zote tano ilizocheza hadi sasa, itashuka Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kesho kuivaa Singida United kwenye muendelezo wa ligi hiyo.

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic