October 12, 2019


Ni kama fitina vile, unaambiwa mabosi wa Pyramids FC ya Misri wameahidi donge nene kwa wachezaji wao endapo wataitoa Yanga kunako Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga na waarabu hao watakutana katika mechi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika kwenye Uwanja wa CCM, Kirumba jijini Mwanza itakayokuwa ni ya kuwania kufuzu hatua ya makundi.

Taarifa zinasema mabosi wa waarabu hao wameahidi donge hilo kama sehemu ya motisha ili Yanga itinge hatua ya makundi ndani ya mashindano hayo.

Timu hiyo inayotajwa kufanya usajili wa mabilioni, mpaka sasa ipo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi wa Misri ikiwa na alama 7 baada ya kucheza mechi tatu ikishinda mbili na mmoja ikienda sare.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic