October 12, 2019


Baada ya kupata kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 10 katika ushindi wa kwanza wa lig dhidi ya Coastal Union, wadhamini wa klabu hiyo, GSM wameahidi kutoa milioni 50 kwa kila mechi endapo Yanga watapata matokeo, imeelezwa.

Fedha hizo zinawekezwa kwa ajili ya kuzidi kutoa morali kwa timu hiyo ili izidi kufanya vema katika mechi za ligi msimu huu.

GSM wameamua kutoa fedha hizo kutokana namna Yanga ilivyoanza ligi kwa kusuasua na inaelezwa dhumuni la kutoa fedha hizo ni kuhakikisha Yanga inatwaa ubingwa msimu huu.

Milioni 50 hizo zinazidi kutia hamasa ndani ya mabingwa hao wa kihistoria kunako Ligi Kuu maana inaonesha hata wadau, mashabiki, wanachama pamoja na wachezaji wamezifurahia.

4 COMMENTS:

  1. Dante unaisikia hiyo offer? Huwezi kuondoka offisini bila kulipwa mshahara,lakini posho na marupurupu yakiwa mengi mshahara utasubiri tuu

    ReplyDelete
  2. kuna mambo mengine unabid unyamaze tuu

    ReplyDelete
  3. Uonevu mtupu na wizi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic