WAMETUPA FUNZO KUBWA LA BURE
Vijana wetu, MALI YETU kwa maana ya hawa ni Wazalendo haswa kwa kuwa ni vijana wa Kitanzania ambao WAMETUDUNDISHA JAMBO.
Jambo lenyewe ni kwamba pamoja na kutafuta wachezaji nje hasa kwa klabu zetu kubwa na zenye uwezo wa kifedha. Basi kuna uwezekano wa KUANGAZA macho hapa nyumbani kwa UTULIVU.
ANGALIA, Yanga wakati wanasubiri akina Karengo, Bigirimana na wengine waamke, tayari Balama kawaonyesha yeye ni ALAMA na anaweza.
Pale Simba wakati wakimsubiri Kanda aonyeshe alichonacho, Miraji Athuman au Sheva, tayari ameanza kufanya yake na yanakubalika.
WAKO kina Sheva na Balama wengi sana wanaoweza kufanya Mapinduzi.
Tena kuonyesha UWEZO wao hauna ZENGWE, wanaowaamini ni makocha kutoka NJE.
Balama na Sheva endeleeni KUSONGA bila ya kulewa SIFA.
0 COMMENTS:
Post a Comment