October 11, 2019



LICHA ya timu ya Yanga kucheza jumla ya michezo mitatu ambayo ni sawa na dakika 270 imeipoteza Simba ambayo imecheza michezo minne ambayo ni sawa na dakika 360 kwa kupata kona chache na kufunga bao.

Kwenye jumla ya michezo mitatu iliyocheza mpaka sasa Yanga imepiga jumla ya kona 16 huku Simba ikipiga jumla ya kona 17 na kwenye kona hizo Simba haijaambulia hata bao la kuotea huku Yanga ikipata bao moja.

Simba ilianza kupiga kona tano kwenye mchezo wake wa kwanza dhidi ya JKT Tanzania na jukumu la kupiga mipira hiyo kuachiwa Clatous Chama, kisha ikapiga kona 6 dhidi ya Mtibwa Sugar, kona 2 kwa Kagera Sugar na kona 4 mbele ya Biashara United ikaambulia patupu.

Yanga ilianza kupiga kona 9 dhidi ya Ruvu Shooting, ikapiga kona mbili mbele ya Polisi Tanzania kabla ya kupiga kona 5 mbele ya Coastal Union ambapo walipata bao la ushindi.

Kona hiyo ilipigwa na Mrisho Ngasa uwanja wa Uhuru na ilipachikwa kimiani kwa kichwa na kiungo Abdulaziz Makame na kuipa Yanga pointi tatu kwa mara ya kwanza baada ya kupoteza mchezo wa kwanza mbele ya Ruvu Shooting na kulazimisha sare mbele ya Polisi Tanzania uwanja wa Uhuru.

8 COMMENTS:

  1. Yaan mm sion kama kna jambo la maana apa simba ina michezo 4 ina point 12 yanga michezo 3 ina point 4 nashangaa mwaandish wa hii blog unashangilia Kona walio funga

    ReplyDelete
  2. Hu ni upuuzi. Simba mechi tatu points9 wakati Yanga mechi tatu points4? Sasa ukimuona mwanamme halisi anasherekea kukonyeza nakuwaacha watu wanaendelee kugonga basi ujue huyo mtu si mzima.

    ReplyDelete
  3. Huyu mwandishi huwa anawaza nini hivi dah blog ya hovyo hii

    ReplyDelete
  4. Saleh Ally do something .Blog yako inapoteza weledi kwa kasi. Ujinga na kulinganisha mambo ya ajabu.
    Kuna mwandishi kanjanja ndio anaiharibu blogu.Uliona wapi watu wanalinganisha kona?Tunangoja mipira ya kutupa na faulo.Naacha rasmi kusoma hii blogu.

    ReplyDelete
  5. Hivi hawa TCRA hawaoni upuuzi wa hii blog?Wanatoza faini vituo na blog zenye kujielewa ambazo zina mapungufu madogo madogo yanayohitaji ushauri tu na kuiacha hii blog inayokera nyoyo za watu na kuchafua tasnia ya habari.

    ReplyDelete
  6. Huwo uyanga wako peleka kwenye gazeti la bingwa ambalo ulifukuzwa tumecheza mechi zote na tumeshinda wewe na hao kandambili wako mlio pewa goli na huyo refa mechi ya polisi mshukuru mungu kama huna cha kuandika futa hii blog yako

    ReplyDelete
  7. Yanga wameipiga bao Simba!!!Mechi tatu pointi 4!!Huko ndio kupiga bao??Kweli uzwazwa na ukandambili unaweza kusema chochote .

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic