ZAHERA ALIPUA BOMU YANGA
Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema hawezi kuwasikiliza Mashabiki wanachokisema kwa sasa baada ya kufungwa na Pyramids FC kwani anawasiliana na Uongozi uliompa Mkataba
Ni baada ya mashabiki wa Klabu hiyo kulalamika wakimtaka Zahera kuondoka kutokana na matatizo wanayodai yamekithiri ikiwemo kushindwa kupanga kikosi na kukosa mbinu
Amesema, "Mimi sikuajiriwa na mashabiki wa Yanga bali nilisaini mkataba na viongozi, kwa hiyo siku viongozi wakinitaka niwaachie timu nitafanya hivyo, sitokwenda mazoezini."
Ameongeza, "Nina uzoefu mkubwa Afrika, mashabiki wanakasirika. Hakuna mchezaji yeyote wa Yanga anayeweza kucheza Pyramids na hatukusajili kwa ajili ya Klabu Bingwa ila ligi."
This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteTATHMINI YA KINA KUHUSU YANGA NA USHAURI
Delete✴Swali:Tatizo ni nini?
☑Jibu: Yanga Kutopata Matokeo Mazuri huku Wakicheza Ovyo na Kutoonyesha Dalili za Kubadilika baada ya Michezo Kadhaa ya Kirafiki (Pre-season) , Ligi, na Ya Kimataifa. Wapenzi, Mashabiki, Wanachama na Wadau wa Timu ya "Wananchi"...wanaumia, kulia, kunung'unika, kulaumu, na kuwa na shida mioyoni kwakuwa Timu yao pendwa....Ina matokeo ya uwanjani "mabovu na yasiyoridhisha" yasiyo wapa raha na matumaini ya leo na kesho. Kinachowaumiza zaidi ni kuwa kelele zao na sauti zao haziheshimiwi na sana sana zinazihakiwa wakati hao wanaofanya hivyo wanashindwa kutambua kuwa...hawahawa wanachi kiuhalisia ndio wanaitwa kuja viwanjani kushangilia Timu, ndio wanaosafiri ndani na nje ya Nchi kuambatana na Timu na kuisapoti Timu. Hawa wananchi ndio wanaochangishana na kuhusika kwenye matukio ya Kubwa Kuliko, Wiki ya Mwananchi nk....katika kukusanya "mtaji" kusaidia kwenye Usajili wa Wachezaji....kinachowauma zaidi ni kujibiwa majibu ya dharau na kebehi na Kocha Mwenye Dhamana ya Kubeba Matumaini Yao.
✴Swali: Yote haya chanzo chake ni nini?
☑Jibu: Sababu ziko Nyingi....unaweza ukazigawa katika maeneo 9
♦Mapungufu katika Benchi la Ufundi (Mbinu, Ufundi, Mifumo, Maandalizi ya Mechi, na Uwezo wa Benchi Zima kuwa Umefikia "UKOMO")...kukosekana kwa Plan B, C, D & E...Katika kukabiliana na Timu pinzani wakati wa mechi ziwe za kirafiki, ligi, na mashindano ya Kimataifa
♦Aina ya Wachezaji Waliosajiliwa..... Viwango Kuporomoka na Kushindwa kuleta Ushindi (Waliotokana na Mapendekezo ya Benchi la Ufundi)
♦Timu Kwa Ujumla wake Kutoonyesha mabadiliko kutoka mechi moja kuelekea nyingine. Timu yoyote itakayocheza na Yanga hii itaweza kuisumbua hata ikiwa ya daraja la pili.....tumeona mifano Pamba, Friends Rangers, Polisi, Mbao, Mawenzi Market nk
♦Kuongezeka kwa Majeruhi kutokana na sababu mbalimbali...aina ya viwanja vya mazoezi, aina ya mazoezi, madhaifu ya kambi na huduma zake, matunzo binafsi ya mchezaji(kuongezeka uzito aina ya vyakula, mazoezi binafsi,) jinsi wanavyocheza kama walivyofundishwa na wanavyozuia timu pinzani (rafu na kadi za njano ni nyingi mno)...hii inapunguza uhalisia wa kuwa na kikosi kipana. Idara ya Utabibu imezorota pia aidha ni uwezo wa kiuchumi wa timu au udhaifu wa kiutawala katika kutafuta suluhisho
⤵
Kutokuwepo kwa Mwalimu Msaidizi....ambaye Kocha Zahera hapo mwanzo amekuwa akilipinga hili huku akijua msaidizi aliyenaye kwasasa Viatu havimtoshi...nayeye kuchelewa preseason trials na camp preparations kutoa visingizio vingi visivyo na mantiki au mashiko
ReplyDelete♦Benchi la Ufundi kujikita kwenye Media, Mitandao na Kujibizana na Waandishi na Vyombo vya Habari, Watawala wa Soka (TFF & Bodi ya Ligi)..badala ya kutumia muda mwingi kukiandaa kikosi na kurekebisha kasoro za timu....
♦Uongozi wa Yanga kukasimu Madaraka Makubwa ya Kiutawala kwa Kocha bila kuweka mipaka ya Taaluma yake....kumekuwa na shida kuelewa taarifa ambazo watawala wanatakiwa kujibu na Taarifa ambazo Kocha anatakiwa kujibu. Kujibu hadharani mambo ya ndani ya Timu na Kuwaexpose wachezaji na mambo yao na kuwashusha morali kutokana na hulka hiyo ya kuweka mambo na udhaifu wao hadharani, kwakuwa wengi bado ni Vijana wadogo wanaathirika kisaikolojia, na wameshindwa kurecover kwa haraka, na mbaya zaidi mitandaoni haya pia wanayasoma. Maadui wametumia mwanya huo kuiadhibu Timu. Kwa tamaduni za wachezaji wa kitanzania hili ni jambo la hatari Kocha kuweka mambo hadharani ambayo si ridhaa ya mchezaji, na familia yake.
♦Watendaji wengine wa Benchi la Ufundi...(Mameneja, Wasaidizi wa Mwalimu, Madaktari) kushindwa kumsaidia na kumshauri Kocha kuhusu namna ya kurekebisha dosari na kasoro zinazoonekana kwenye mazoezi na mechi....wakiamini kuwa Mwalimu anajua kila kitu. Upeo wa Kocha unaweza ukawa umefikia kikomo lakini kwakuwa hii ni Timu na ndiyo sababu ya kupewa wasaidizi wamsaidie lakini hakuna matokeo chanya kuonyesha Mabadiliko yanakuja kutokana na uwepo wa wasaidizi wa mwalimu wao wanafanya vilevile anavyoona mwalimu na falsafa yake hata kama haijaweza kusaidia Timu kupata ushindi
♦Mwalimu Zahera ni mwalimu wa Saikolojia lakini si mwalimu mwenye mbinu za soka za kuleta ushindani na kusoma mapungufu ya timu pinzani na kuyafanyia kazi....wachezaji wa kitanzania, hawatakiwi tu kujengwa kisaikolojia bali pia wanatakiwa waelimishwe mbinu kwasababu wengi wao misingi ya soka siyo imara kama ambavyo Kocha anataka kuamini (sio ready-made players)⤵
Uongozi na Utawala:
ReplyDeleteA: Kamati iliyoundwa imepewa mipaka lakini imeshindwa kuleta mabadiliko ya kumshauri mwalimu ingawa muda ni mfupi tokea iteuliwe
B: Uwekezaji na Mabadiliko ya Uendeshaji:
mpira ni pesa matokeo mazuri ya uwanjani yanachangiwa na sababu nyingi....mojawapo ni pesa ambayo itasaidia kuwekeza
1.Muundo wa Uendeshaji wa Kisasa: Ambapo kwa sasa umekuwa ukienda taratibu au hata haujaanza
2. Kutafuta Mkurugenzi wa Ufundi na Mwalimu Msaidizi Benchi la Ufundi
3. Kuongeza wachezaji mahiri na kupunguza wachezaji wasio na tija....kulipa madeni ya wachezaji wa zamani na waliopo, kuvunja mikataba kwa walimu na wafanya kazi wasio na tija
✴Swali: Je ni muda muafaka wa Kuleta Mabadiliko ya Kocha?
☑Jibu: Kwa mtazamo wangu...inategemea hali ilivyo kwasasa (trend ya team uwanjani)....lakini kwa jibu rahisi kwakuwa ligi ndio imeanza NAFIKIRI MABADILIKO YA KOCHA YANAWEZAKANA...yafuatayo yanaweza kufanyika
Anaweza akaajiriwa kama Mshauri wa Ufundi kwanza akipewa mkataba mfupi wa siku 90....ili aiangalie na kuiassess timu akiwa mshauri pekee wa Zahera na ndiye atakaependekeza kusajiliwa ama kuachwa kwa makocha au baadhi ya wachezaji wasio na tija. Huku taratibu za kuachana na Zahera na Mwandila au Zahera pekee, zikifanyika taratibu kwa kufuata mikataba iliyopo. Huyu Mshauri aanze kufundisha rasmi baada ya dirisha dogo la usajili kumalizika
Ahsanteni
mbona hatukuziona hoja kama hizi wakati simba walipotolewa raundi ya kwanzaaaa!!!
ReplyDeletekila mtu anajifanya anajua!! au yanga imekua kicha cha mwendawazimu kila mtu anajifundishia kutoa hoja kupitia kwao !!
hawa Piramid ndio wanaowafunga Al Ahly kila mwaka na wanao wachezaji 8 wa timu ya taifa misri, hivyo kufungwa 2-1 si jambo la ajabu sana kwa timu kama hii
ReplyDeleteMsema kweli
ReplyDelete