JAMIE Vardy nyotawa Leicester City alifungua akaunti ya mabao mbele ya Arsenal kwenye mechi yao ya 12 ndani ya Premier League mbele ya Arsenal.
Bao lake ambalo lilisubiri mpaka dakika ya 68 lilidumu kwa dakika saba ambapo bao la pili lilipachikwa dakika ya 75 na James Madison.
Ushindi huo wa mabao 2-0 unaifanya Leicester City kushika nafasi ya pili ikiwa na pointi zake 26 kibindoni kwa sasa ikiachwa kwa pointi tano na Liverpool ambao ni vinara.
Pia ipo mbele kwa mchezo mmoja ikiwa imecheza mechi 12 tofauti na Liverpool ambayo imecheza mechi 11 na pointi zake 31.
Arsenal sasa inashika nafasi ya sita ikiwa na pointi zake 17 baada ya kucheza mechi 12 ndani ya Ligi Kuu England.
0 COMMENTS:
Post a Comment