November 13, 2019


Aliyekuwa rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na wenzake wawili,  wataanza kujitetea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Novemba 20 mwaka huu.

Mbali na Aveva wengine ni aliyekuwa makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Godfrey Nyange (Kaburu),  na aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili, Zachariah Hans Pope.

Wakili wa Serikali, Silvia Mitanto, aliieleza mahakama hiyo kuwa wanaomba tarehe ya kutajwa ili weweze kuendelea na rufaa waliYokata katika Mahakama Kuu ya Tanzania ya kupinga maamuzi yaliyotolewa na mahakama hiyo kuwaondolea mashtaka ya utakatishaji wa fedha washtakiwa Aveva na Nyange.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alisema:  “Upande wa mashtaka kama mmekata rufaa mtaendelea lakini mahakama hiyo itaendelea na usikilizwaji wa utetezi.”

Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 20, 2019,  itakapokuja kwa ajili ya kusikiliza utetezi.

Katika rufaa hiyo Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), amepinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwaondolea Aveva na Kaburu mashtaka ya utakatishaji fedha na kuwapa masharti ya dhamana.

Katika kesi hiyo, Aveva na Nyange walikuwa wakikabiliwa na mashtaka tisa ambapo Septemba 19 mwaka huu mahakama hiyo iliwaondolea mashtaka mawili ya utakatishaji fedha kwa kuwa upande wa mashtaka ulishindwa kuyathibitisha.

Hata hivyo, Mahakama hiyo iliwakuta na kesi ya kujibu katika mashtaka saba ambayo ni kughushi, kula njama, matumizi mabaya ya madaraka, kutoa nyaraka za uongo, na kutoa maelezo ya uongo ambayo upande wa mashtaka umeweza kuyathibitisha.

Katika shtaka la kwanza, Aveva na Kaburu walikula njama ya kutenda kosa la matumizi mabaya ya madaraka ambapo katika shtaka la pili Aveva na Nyange wanadaiwa kutumia vibaya madaraka yao kwa kuandaa fomu ya kuhamisha fedha ambazo ni Dola za Kimarekani 300,000 kutoka kwenye akaunti  iliyoko benki ya CRDB Azikiwe kwenda kwenye akaunti binafsi ya Aveva iliyoko benki ya Barclays.

Shtaka la tatu linalowakabili Aveva na Nyange ni kwamba wanadaiwa kwa pamoja kughushi nyaraka iliyokuwa ikionyesha  Klabu ya Simba inalipa mkopo wa Dola za 300,000 kwa Aveva kitu ambacho si kweli.

Katika shtaka la nne,  inadaiwa katika benki ya CRDB, Aveva anadaiwa kutoa nyaraka ya uongo ikionyesha Simba wanalipa mkopo wa Dola za Kimarekani 300,000.

Shtaka la tano linawakabili Aveva, Kaburu na Hans Poppe ambao wanadaiwa kughushi hati ya malipo ya kibiashara wakionyesha kwamba nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zina thamani ya Dola za Kimarekani 40,577 huku wakijua kwamba si kweli.

Katika shtaka la sita, Aveva anadaiwa kuwasilisha hati ya malipo ya kibiashara ya uongo kwa Levison Kasulwa kwa madhumuni ya kuonyesha kwamba Simba wamenunua nyasi bandia zenye thamani ya Dola za Kimarekani 40,577.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic