November 13, 2019


Ikiwa ni siku kadhaa zimepitwa tangu kupigwa chini kwa aliyekuwa Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, Mkongomani huyo inaelezwa anaweza akapata dili katika timu ya AS Vita.

Uwepo wa taarifa hizo zinakuwa kama zinawaumbua Yanga ambao waliachana naye na itakuwa kama bahati kwa Zahera kupata dili hilo endapo atasajiliwa kuwa Msaidizi wa Florent Ibenge ambaye ndiye Kocha Mkuu.

Taarifa zinasema Rais wa Vita Club, Gabriel Amissi amesema bado anashauriana na kocha mkuu wa klabu yake, Ibenge kumpa ofa Zahera.

Ikumbukwe hivi karibuni Vita Club iliwafuta kazi makocha wasaidizi wote, Ibenge na Zahera walishawahi kufanya kazi kwa pamoja kwenye timu ya Taifa ya Congo DR.

5 COMMENTS:

  1. Tulisha sahau sisi huyo ..................

    ReplyDelete
  2. huyu saleh bila kumuandika zahera hauzi gazeti, na hawa ndio walichangia kuondoka kwa zahera kwan walimfanya akose muda wa kufikir maendeleo ya timu uwanjani na hatimae kufikir lini na ataongea nn na media.
    nenda zako saleh huna mpya

    ReplyDelete
  3. Sasa anawaumbua vipi Yanga wakati kule kama ni kweli anachukuliwa kuwa kocha msaidizi?

    Maana yake hatakuwa na maamuzi ya mwisho na wala mbinu zake siyo zitakazotumika ktk club hiyo.

    Yaani mwanzo nilikuwa naamini hiki ki blog lkn kumbe ni waganga njaa tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Well said ndugu, hata Kama akiajiriwa Kama kocha Mkuu timu nyingine huwezi kusema kaiumbua Yanga...Yanga haijamfungia Zahera ukocha, Bali kwa Sasa amekosa sofa kugundisha Yanga.

      Delete
  4. huyu Salehe FALA mimi kila siku nasema

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic