Baada ya kurejea leo akitokea Cairo, Misri ambako alikuwa na kibarua cha kuiongoza Yanga katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids FC, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera ameshangazwa na ratiba ya ligi.
Zahera ameelezwa kushangazwa baada ya kupata taarifa kuwa watakuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara Ijumaa ya wiki hii dhidi ya Ndanda FC ambapo watapaswa kusafiri kwenda Mtwara.
Kocha huyo ambaye ni raia wa Congo, ameeleza kuwa alikuwa hana taarifa kabisa juu ya uwepo wa mchezo huo jambo ambalo limemshangaza.
Akizungumza mara baada ya kutua Uwanja wa Ndege, Zahera amezungumza akiwa anajua watakuwa na siku kadhaa za kupumzika kutokana na safari ya kutoka Misri.
Kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Pyramids FC hapo jana kimewaondoka rasmi Yanga kunako mashindano hayo na wapinzani wao wakiingia hatua ya makundi.








Hakika huyu kocha hajielewi kabisa, Misri kuna umbali gani? Jana Jumapili saa tatu usiku kacheza game na leo Jumatatu kafika bongo na timu yake, anapewa ratiba ya kucheza IJUMAA, inamaana anapumzika JUMANNE, JUMATANO na ALHAMIS siku 3, bado analalamika kanyimwa siku za kupumzika?
ReplyDeleteHuyu afunge virago zake.Yanga watafute kocha mpya.Hata ligi kuu wasiwasi
ReplyDeleteHongera kwa Yanga lazima wale viporo
ReplyDeleteDawa ya Mgonjwa ni kufanya upasuaji ili kuondoa kiini cha ugonjwa sio kumpatia chakula ukitegemea kiini kitaondoka....Tatizo ni benchi la ufundi limefikia ukomo wa uwezo hiki ndicho chanzo cha mashabiki kushinikiza kuondolewa kwa Kocha au Mabadiliko kufanyika. Hata ukisajili akina Messi na Ronaldo kama ufundishwaji ni poor usitegemee ushindi. Yanga hii inahitaji uwekezaji bora ambao unaendana sambamba na benchi la ufundi lililo bora....Uongozi wa Yanga unajivutavuta na kujificha kwenye kichaka na kivuli cha Zahera lakini ukweli ni kuwa Kocha huyu hatawafikisha popote....mbinu zimegota...
ReplyDeleteHa ha ha ha ha acheni hekima itawale,huyu ni kanjanja amekuja kuimaliza timu endapo yanga hawatamfukuza basi atakuja kuingamiza timu mazima.god bless yanga.
ReplyDeletewakati anaeenda misri ratiba ilikuwepo sasa anshangaa nini
ReplyDelete