November 15, 2019


Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, ameibuka na kumpiga dongo kiaina kwa mfumbo Haji Manara ambaye ni Msemaji wa Simba kutokana na kuizungumzia Yanga mara kwa mara.

Bumbuli amesema kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiizungumzia Yanga kila wakati badala ya kutimiza majukumu yao yanayowahusu.

Kutokana na kauli hiyo, Bumbuli amewataka wanayanga wote kutoyumbishwa na watu wa aina hiyo na badala yake waungane kwa ajili ya kuijenga timu yao.

Mapema jana asubuhi, Manara aliibuka na kuzungumzia sintifahamu iliyojitokeza juu ya Bumbuli na Ofisa Mhamasishaji, Antonio Nugaz kuwa wote wanajiita wasemaji wa Yanga.

Katika andiko hilo dogo lililoambatana na sauti za Nugaz na Bumbuli, Manara alisema wawili hao lengo lao si usemaji ndani ya klabu bali ni kushindana naye kupata umaarufu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic