November 14, 2019


Mdau na mwanasoka wa zamani hapa nchini, Kenny Mwaisabula maarufu kama Mzazi, amefunguka kwa kusema kuwa wachezaji wengi wa kigeni wanafeli kutokana na kuendekeza starehe.

Mwaisabula ameeleza wachezaji wengi kutoka nje ya nchi wamekuwa wakifika nchini wakiwa na viwango vizuri lakini baada ya muda wanapotea kwenye ramani.

Mdau huyo amemtaja mchezaji wa Simba, Mzambia, Clatous Chama, kuwa ni moja ya wachezaji ambao kwa sasa hawana makali kama alivyotua wakati anatokea Power Dynamos ya Zambia.

Ameeleza kuwa starehe imemgharimu Chama na sasa hana tena ule umaridadi ndani ya dimba kitu ambacho kimesababisha kiwango chake kuporomoka.

"Chama ninayemfahamu mimi si yule wa Simba aliyekuwa mzuri kwa mwaka jana, wachezaji wengi wa nje wakija Tanzania hawamalizi mwaka mmoja wanapotea dimbani, starehe wanaendekeza zaidi kuliko kazi",

3 COMMENTS:

  1. Kweli kabisa...Chama amejiingiza kwenye starehe na nina imani kuna baadhi ya wachezaji wa kibongo wanahusika..Chama yuko karibu sana na Mkude na ni ukweli Mkude nae kwa starehe hajambo.. Tumeona watu kama Zana aliporomoka kiwango kwa muda mfupi wakati kuna watu kama Kagere na Okwi wao kiwango chao kimedumu bila kushuka.

    ReplyDelete
  2. Acheni uongo mlimkuta wapi anafanya starehe,!!!??

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic