NYOTA wa timu ya Juventus inayoshiriki Serie A, Cristiano Ronaldo amewaomba mabosi zake wampe mkataba kiungo wao wa zamani Paul Pogba ambaye kwa sasa anakipiga Manchester United ndani ya Premier League.
Pogba ambaye timu yake ya Ufaransa ni mabingwa wa kombe la Dunia, uwezo wake umekuwa ni wa kusuasua ndani ya Old Trafford kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.
Real Madrid inayoshiriki La Liga imekuwa ikitajwa kuiwania saini ya nyota huyo huku kocha wao Zinedine Zidane akisema kuwa ni miongoni mwa viungo anaowakubali wakiwa uwanjani.
Mabosi wa United wametaja dau la kukomoa kwa timu inayotaka saini yake ambayo inatajwa kuwa ni pauni milioni 80 na Juventus wanatajwa kuongeza juhudi ili kuinasa saini yake ifikapo mwezi januari.
0 COMMENTS:
Post a Comment