November 18, 2019


KOCHA mwenye heshima kubwa nchini DR Congo na ukanda wa Cecafa, Raoul Shungu amelithibitishia Spoti Xtra kwamba Yanga wamempigia lakini mshahara aliowatajia hautofautiani parefu na Patrick Aussems wa Simba.

Shungu ambae ni miongoni mwa makocha wanaolipwa vizuri nchini humo, ameweka wazi kwamba Yanga wamemwambia wanataka kumpa timu na yeye yuko tayari hata sasa hivi.

Kocha huyo ambaye kwa sasa ni Msaidizi wa bosi AS Vita, Florent Ibenge(swahiba na jirani wa Mwinyi Zahera nchini Ufaransa), amewaambia Yanga anataka mshahara wa Sh.Mil 25 ambazo zitamfanya awe kocha wa pili kwa kukinga mshahara mnono kwenye Ligi Kuu Bara.

Kocha wa Simba, Patrick Aussems ndiye anayeongoza kwani analipwa Sh.Mil 27.5, kwani Mbelgiji huyo alipandishiwa kiasi hicho kwenye mkataba mpya aliosaini hivi karibuni. “Nilizungumza na kiongozi mmoja mkubwa wa Yanga na mazungumzo yetu yalikuwa yanahusu kuja kuifundisha timu hiyo, tulizungumza mambo mengi.

“Nilimwambia kuwa nahitaji milioni 25 kila mwezi ili niweze kufanya kazi yangu kwa umakini, aliniambia anakwenda kujadiliana na wenzake atanirudia lakini ninachoshangaa baada ya hapo imekuwa kimya kabisa,”alisema Shungu ambae Mkongo mwenzie aliyetimuliwa Mwinyi Zahera alikuwa analipwa Sh.Mil 7.

“Kama kweli wananihitaji basi wanitafute tena tuongee kwani ni makubaliano tu, halafu isitoshe mimi nilishawahi kuwa kocha pale, nakumbuka nilikuwana marafi ki zangu mitaa ya Magomeni hivyo kama wananihitaji wajetena tuzungumze zaidi maana kuna timu nyingine pia zinanihitaji,” alisema kocha huyo ambaye habari za ndani zinasema kwamba hataki kuendelea kufundisha AS Vita. 

Raoul Shungu aliwahi kuipa Yanga ubingwa wa Ligi Kuu mwaka 1998 ambapo mwaka 2001 aliondoka katika klabu hiyo na nafasi yake ikachukuliwa na Boniface Mkwasa ambaye kwasasa amepewa nafasi ya kukaimu.

MAKOCHA WENGINE

Mbali na Shungu ambaye anakubalika na viongozi wengi wa kamati ya ufundi ya Yanga, wapo makocha wengine wanaowindwa na Yanga. Yupo Mholanzi,Lodewjik de Kruif Jorvan Viera mwenye uraia wa Brazil na Ureno na Mfaransa Didier Gomes da Rose ambaye pia alikuwa akiifundisha Horoya AC ya Guinea anakosuguabenchi Heritier Makambo ‘Mzee wa kuwajaza’. Makocha wengine ni Mholanzi Ernie Brandts na Mserbia Nicola Kavazovic na Kostadin Papic.

Brandts na Papic waliwahi kuifundisha Yanga na kuipa mafanikio ya kawaida sana. Leo kamati ya utendaji ya Yanga inakutana kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali ikiwemo ishu ya Kocha na usajili wa dirisha dogo.

Makamu mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela alipoulizwa kuhusiana na ishu ya kocha alisema kuwa : “taratibu za kumpata kocha mpya zinaendelea lakini kwa sasa siwezi sema tumefi kia wapi ila bado. Muda utakapofi ka kila kitu kitakuwa wazi na kila mtu atajua.”

Lakini hata hivyo, mmoja wa vigogo wa Yanga ameidokeza Spoti Xtra kwamba kuna uwezekano wakamwachia Mkwasa timu amalize msimu huu kwa vile wanashiriki mashindano ya ndani tu.

CHANZO: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic