PEP Guardiola, Kocha wa Manchester City amewekwa kwenye rada na timu ya Bayern Munich ili akachukue nafasi ya Niko Kovac.
Miamba hiyo ya Bundesliga inaamini kuwa ikiwa itampata Thomas Tuchel wa PSG na Erick ten Hag (Ajax) itakuwa bora lakini wakimpata bosi huyo wa Manchester City itakuwa bora zaidi.
Miamba hiyo ya Bundesliga inaamini kuwa ikiwa itampata Thomas Tuchel wa PSG na Erick ten Hag (Ajax) itakuwa bora lakini wakimpata bosi huyo wa Manchester City itakuwa bora zaidi.
Kwa sasa Guardiola bado ana mkataba na mabosi zake wanaoutumia Uwanja wa Etihad mpaka 2021 licha ya Bayern Munich kuamini kwamba wanaweza kumshawishi kurejea Allianz Arena msimu ujao baada ya miaka minne kupita.
Miezi michache iliyopita, iliripotiwa kuwa bosi huyo alitembelea sehemu ya mazoezi ya Bayern ambayo alikuwepo hapo zamani.
0 COMMENTS:
Post a Comment