GUINEA KUPIGWA KILAINI NA STARS IJUMAA
IJUMAA Novemba 15, mwaka huu, timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars itamenyana na Equatorial Guinea kwenye mchezo wa kuwania kufuzu tiketi ya kuwania kushiriki michuano ya Afcon inayotarajiwa kufanyika 2021.
Kwenye jumla ya mechi nne za ushindani ambazo timu hiyo ya Taifa ya Equatorial Guinea imecheza, hakuna hata moja ambayo wameambulia ushindi zaidi ya kupata sare na vichapo wakiwa ugenini tofauti na Stars ambayo imeambulia ushindi ikiwa ugenini mbele ya Sudan kwa kuifunga mabao 2-1.
Guinea Ilipoteza mbele ya timu ya Taifa ya Congo kwa kufungwa bao 1-0, pia ililazimisha sare ikiwa nchini Sudan Kusini ya kufungana bao 1-1, pia dhidi ya Chad kwa sare ya mabao 3-3, na iliambulia kichapo mbele ya Saudi Arabia kwa kufungwa mabao 3-2.
Kwenye jumla ya mechi nne ikiwa ugenini, imefungwa mabao nane huku wao wakifunga mabao sita pekee.
Kocha Msaidizi wa Stars, Juma Mgunda, ameliambia Championi Jumatano kuwa wanatambua ugumu wa mchezo ila watapambana kupata matokeo.
“Tunatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu lakini tutapambana kupata matokeo, mashabiki wajitokeze kwa wingi kutusapoti.”
Uchambuzi maandazi kwani karibu wachezaji wote wa kutegemewa wa equatorial guinea wanaishi nje ya Taifa lao na mara nyingi hurejea kuichezea timu yao ya taifa kunako mechi za ushindani za kimashindano kwa hivyo kujidanganya kuwa timu hiyo ni kibonde kwa Taifa stars basi ni sawa na kujenga mazingira ya kuiondoa Taifa stars kwenye kampeni za kufuzu can .
ReplyDelete