HOSPITALI YATEKETEA KWA MOTO
HOSPITALI ya Mombasa nchini Kenya imeteketea kwa moto, huku wagonjwa wakiokolewa na hakuna majeruhi wowote.
Imeelezwa kwamba moto huo ulizuka katika Hospitali hiyo yenye uwezo wa kulaza wagonjwa 125 majira ya saa 2:30 usiku wa kuamkia leo ambapo wauguzi 117 walikuwa hospitalini hapo wakiendelea na majukumu yao.
Baada ya wagonjwa kuokolewa walikimbizwa katika hospitali jirani za Pandya, Aga Khan na Hospitali ya Coast General.
Kwa mujibu wa Kikosi cha Zimamoto, chanzo cha moto huo ulioanzia katika chumba cha watoto bado hakijafahamika.
0 COMMENTS:
Post a Comment