November 28, 2019


Wasanii wa Tanzania, Alikiba na Harmonize watakutana katika jukwaa moja la tamasha la Fiesta litakalofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Desemba 8, 2019.

Waandaaji wa tamasha hilo juzi Jumanne Novemba 26, 2019 wametangaza baadhi ya wasanii nchini watakaoshiriki Fiesta, wakiwemo wawili hao.

Kukutana jukwaani kwa wasanii hao kunasubiriwa kwa hamu kutokana na Harmonize kuachana na lebo ya Wasafi, hivyo mashabiki wengi kutaka kumshuhudia akitoa burudani nje ya lebo hiyo.

Jana Alhamisi ya Oktoba 24, 2019, Harmonize alieleza jinsi alivyouza nyumba zake tatu na baadhi ya mali ili kuilipa lebo ya Wasafi Sh500 milioni kwa ajili ya kupata hakimiliki ya kutumia nyimbo zake na jina.

Alibainisha kuwa mkataba alioingia na lebo ya Wasafi inayomilikiwa na msanii Diamond Platnumz ilikuwa na kipengele cha kulipa kiasi hicho cha fedha ikiwa atavunja mkataba ili aweze kuendelea kutumia nyimbo pamoja na jina lake la kisanii.

Wakati akiwa Wasafi, Harmonize hakuwahi kushiriki tamasha la Fiesta tofauti na Ali Kiba aliyewahi kushiriki mara kadhaa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic