November 3, 2019


JUMA Mwambusi, Kocha Mkuu wa Mbeya City amesema kuwa anachokifanya kwa sasa ni kukijenga kikosi kipya kitakacholeta ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara.

Mwambusi leo ataongoza kikosi chake kumenyana na Simba uwanja wa Uhuru utakaopigwa leo Novemba 3.

"Kikubwa ambacho tunakifanya kwa sasa ni kujenga kikosi imara kitakacholeta ushindani tunatambua kwamba hatujaanza vizuri ligi.

"Ushindani kwenye ligi ni mkubwa na wachezaji wanatambua kwamba ligi ina mechi nyingi za kucheza wanapaswa wapambane," amesema.

Mbeya City imecheza jumla ya mechi 8 za ligi na imekusanya jumla ya pointi 8 ikiwa nafasi ya 16.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic