GEORGE Kavila nahodha mkongwe kuichezea Ligi Kuu Bara ambaye amedumu kwa muda mrefu ndani ya Kagera Sugar amesema kuwa uwekezaji kwenye soka utainua soka la ndani na kulifanya liwe na ushindani zaidi.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kavila amesema kuwa kila siku ndani ya soka kumekuwa na mabadiliko jambo ambalo linaleta ushindani kwenye.
"Ukubwa uliopo wa soka kwa sasa ni ushindani mzuri unaoendelea na kila mchezaji anapambana kuwa bora, kwa soka letu la Tanzania lipo sehemu ya kati si mbaya wala sio nzuri sana hivyo ni lazima lipige hatua kutoka hapa tulipo.
"Vipaji vipo mikakati makini ikiundwa na kuendelea kuwekeza kesho tutakuwa na wachezaji wengi watakaocheza nje ya nchi zaidi ya hawa tulionao sasa," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment