November 8, 2019



IDD Cheche, Kocha Msaidizi wa timu ya Azam FC amesema kuwa hesabu za kupata pointi tatu leo mbele ya Biashara United zipo miguuni mwa wachezaji wakiongozwa na safu ya ushambuliaji iliyo chini ya Obrey Chirwa na Donald Ngoma.

Azam FC leo itamenyana na Biashara United uwanja wa Azam Complex ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya bila kufungana na Kagera Sugar uliochezwa uwanjani hapo wikiendi iliyopita.

Akizungumza na Saleh Jembe, Cheche amesema kuwa tatizo kubwa lipo kwenye suala la umaliziaji nafasi wanazozitengeneza jambo lililowafanya watumie muda mwingi kuwapa makali washambuliaji wake.

"Tatizo ndilo ambalo tunalifanyia kazi siku zote kwenye nafasi ya ushambuliaji, jambo la kwanza tumekuwa tukicheza mechi za kirafiki kuwaongezea kujiamini na kuongeza ukaribu kwa washambuliaji ikiwa ni pamoja na Ngoma pamoja na Chirwa.

"Imani yetu ni kuona tunapata matokeo mbele ya Biashara United ndio maana tumewapa kazi kubwa washambuliaji na tunahitaji pointi tatu muhimu mashabiki watupe sapoti," amesema Cheche.

Mchezo wa Leo utakuwa wa tatu kwa Kocha Mkuu Arstica Cioaba raia wa Romania kukaa kwenye benchi alionja joto ya kupoteza kwa Ruvu Shooting kwa kufungwa bao 1-0 na sare mbele ya Kagera Sugar.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic