November 8, 2019



KIPIGO ilichokobali Singida United iliyo chini ya Ramadhan Nsanzwurimo mabao 5-1 mbele ya Lipuli kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa juzi Uwanja wa Samora kinaifanya Singida United kuwa timu ya kwanza kupigwa mabao mengi kwenye mchezo mmoja.

Ikiwa imecheza jumla ya mechi 11 Sawa na dakika 990 imeambulia pointi nne pekee ikiwa nafasi ya 20 na kufunga jumla ya mabao matatu bila kuonja ladha ya ushindi msimu huu.

Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa maumivu wanayopitia kwa sasa ni makubwa ila watapambana kurejea kwenye ubora wao.

"Tunapata tabu sana kwa sasa na tunatambua kwamba mashabiki wanaumia ni suala la muda tu kurejea kwenye ushindani kwa sasa tunaomba sapoti tu hamna namna.

"Mwalimu anafanya kazi kwa juhudi kufanya wachezaji waweze kujiamini kwani wanasumbuliwa na hofu wakiwa uwanjani isitoshe bado kikosi kinatengenezwa tunaamini tutafanya vizuri na  tumewaahidi motisha wachezaji wakishinda kwenye mechi," amesema Katemana.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic