Straika Meddie Kagere wa Simba, sasa ni kama amefungwa gavana maana imefikia dakika 90 bila ya kuachia miguu au kichwa chake na kutikiza nyavu.
Michezo miwili ya mwisho ambayo mshambuliaji huyo ameichezea Simba Uwanja wa Taifa hajaifungia timu hiyo bao lolote ikiwa siyo kawaida yake msimu huu.
Kwenye mabao nane ambayo Kagere amefunga mpaka sasa mabao manne amefunga kwa guu la kulia huku mawili akifunga kwa guu la kushoto na mawili kwa kichwa mara ya mwisho kufunga ilikuwa mbele ya Mbeya City wakati Simba ikishinda mabao 4-0, akifunga kwa guu la kulia kwa penalti iliyosababishwa na Miraj Athuman ‘Sheva’.
Mabao hayo Kagere amezifunga JKT Tanzania wakati Simba ikishinda mchezo wake wa kwanza mabao 3-1, alifunga mawili kwa guu lake la kulia akitumia pasi za mwisho za Mzamiru Yassin, mbele ya Mtibwa Sugar alifunga bao moja kwenye ushindi wa 2-1 akimalizia pasi ya Sharaf Shiboub.
Mengine mawili alifunga mbele ya Kagera Sugar ambapo bao moja alifunga kwa kichwa akimalizia pasi ya Shomari Kapombe na moja kwa penalti iliyosababishwa na Miraj kwa guu lake la kulia. Lingine la kichwa alifunga mbele ya Azam FC Uwanja wa Taifa kwenye ushindi wa bao moja akimalizia pasi ya Francis Kahata.
Pia aliifunga Biashara United kwa guu lake la kushoto akimalizia pasi ya Miraj wakati Simba ikishinda mabao 2-0 Uwanja wa Karume na bao lake la nane lilikwamia Uwanja Uhuru wakati Simba ikishinda mabao 4-0 mbele ya Mbeya City mpaka sasa Simba ikiwa imecheza mechi mbili sawa na dakika 180 hajafunga bao wala kutoa pasi ya mwisho.
Kagere amesema kuwa hatazami ni nani anafunga kwenye timu yake anachojali ni kuona timu yake inapata ushindi na pointi tatu muhimu.
“Mimi sitazami nani kafunga na nani kafanya nini, bali ninachoangalia ni timu kupata ushindi,” alisema staa huyo.
Kagere afungukia tuzo za Afrika
0 COMMENTS:
Post a Comment