November 20, 2019


.
·       
  JOSE Mourinho amerejea kwenye kazi ya kuwa kocha mkuu baada ya kupita siku 338 alipotimuliwa kukinoa kikosi cha Manchester United kutokana na mwenendo mbovu wa kikosi hicho ndani ya Ligi Kuu England.

 Hivi sasa amepewa kazi na mabosi wa Tottenham Hotspur akichukua mikoba ya Mauricio Pochettino.
·          
·         Mourinho amepewa mkataba unaomalizika msimu wa 2022/23 akipokea mikoba ya Pochettino ambaye alidumu ndani ya Spurs kwa muda wa miaka mitano akiwa ni kocha mkuu.

Mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy amesema kuwa walikubaliana na bodi kuachana na kocha huyo kwa kile walichohofia kushuka daraja jumla msimu huu kutokana na mwendo mbovu wa timu.

Pochettino ameiacha timu ikiwa nafasi ya 14 kwenye Ligi Kuu England ikiachwa kwa jumla ya pointi 20 na Liverpool huku ikishinda jumla ya mechi tatu pekee msimu huu.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic