November 6, 2019


Beki wa Simba anayepanda na kushuka, Shomari Kapombe, amefichua siri ya yeye na wachezaji wenzake wawili kuondoka Azam FC kwa mpigo kisha kuelekea unyamani.

Ikumbukwe wakati Kapombe anaondoka Azam aliondoka sambamba na Aishi Manula, Erasto Nyoni, John Bocco waliokuwa wakikipiga mitaa ya Chamanzi.

Kapombe ameibuka na kusema kila mchezaji aliondoka kwa utaratibu wake kutokana na makubalino yao na Simba.

Ameeleza kuwa hakuna mpango wowote uliofanyika kwa wao kuondoka kwa mpigo bali kila mtu alifanya mazungumzo kivyake na mabosi wa Simba.

"Ujue kila mtu pale aliondoka kwa utaratibu wake, si kweli kuwa kuna mpango ulisukwa ili sisi sote tuelekee Simba.

"Simba walifanya mazungumzo na kila mchezaji na ndiyo maana wote tukajikuta tuko hapo," alisema Kapombe wakati anafanya mahojiano na kipindi cha Sports Extra ya Clouds FM.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic