SELEMAN Msindi, maarufu kama Afande Sele amesema kuwa yale alyoyaimba kwenye wimbo wake wa Karata dume yametimia na mwanae amefaulu kidato cha sita anakwenda Chuo Kikuu.
Akizungumza na Saleh Jembe, Afande Sele amesema kuwa ni jambo la kheri yale aliyoyaandika na kuyaimba kutimia.
"Kiteto mwanagu Tundajema amesoma, akajiunga na jeshi la JKT majibu yakatoka akafaulu kwenda chuo cha Sokoine na anasoma masuala ya Sayansi ni furaha kwangu na kwake pia yametimia yale niliyoimba kwenye wimbo wangu wa Karata dume.
"Kwa mwendo huu mwanangu Tunda atasoma mpaka chuo Kikuu na Mungu akijalia atafika mpaka East Zuu.
"Siendi mnandani kufuata nyama bali nakwenda Bungeni kueleza machungu ya Muziki huu mana alituahidi bwana mkuu," amesema Sele.
Huyu Afande Sele wacha wenye kumuona kuwa mporokaji lakini kwa wenye kupima udhani wa neno kwa keno kutoka kwenye vinywa vya watanzania walio wengi basi tunajua Afande sele haropoki bali ni miongoni mwa watanzania wenye upeo mkubwa zaidi wa kujua mambo ila ufinyu mdogo wa kujua mambo kwa watanzania wengi hasa kwa wale ambao akili zao zimeoza kabisa kwenye siasa za kipinzani ndio wanaojaribu kum'bomoa Afande Sele ila yupo vizuri na azidishe uzalendo wake wala asirudi nyuma kwani watanzania ni watu wa kupelekeshwa na fitina za nje ya nchi na bila ya kuwa na watu wa kupambana na fitina hizo kama akina Afande Sele na Musiba basi Tanzania tutaingia kwenye dimbwi la akina Libya muda si mrefu .
ReplyDeleteHongera sana
ReplyDelete