November 22, 2019


Mechi ya kwanza ya timu ya Taifa ya Tanzania ilikuwa na ushindani mkubwa ambapo ilimenyana na Equatorial Guinea uwanja wa taifa mashabiki waliona namna mambo yalivyokuwa.

Kuanza kwa ushindi nyumbani kumeamsha ari ya mashabiki kuendelea kuipa sapoti timu yao kwani ilifanya kazi kubwa kupindua matokeo uwanja wa nyumbani licha ya kuanza kufungwa kipindi cha kwanza.

Bado tunaona kwamba makosa yapo yale madogomadogo ambayo yamekuwa yakijirudia kwa wachezaji wetu kushindwa kujiamini wakiwa eneo la hatari.

Wakati mwingine tukiwa nyumbani kwenye mechi zote za ushindani tunapaswa tufunguke mwanzo mwisho huku tukijilinda kwa tahadhari kwani mashabiki wetu wapo pamoja nasi.

Ushindi mliopata ni mbegu kwa ajili ya mechi nyingine ambazo zitachezwa uwanja wa taifa kwani ule mwiko wa matokeo mabaya umekwenda jumla na maji na sasa ni mwendo wa kujiandaa na mechi nyingine uwanja wa taifa.

Kibarua cha pili mbele ya Libya ambao ni mwendelezo wa michuano ya kutafuta matokeo ya kusaka tiketi ya kufuzu Afcon 2021 Cameroon mambo yalikuwa magumu na ni jambo la msingi kujifunza.

Makosa yaliyofanywa yanapaswa yafanyiwe kazi ili kuendelea kupata matokeo chanya kwenye mechi zinazofuata mlima bado ni mrefu na kazi bado ni ngumu hatupsawi kubweteka kwa sasa.


Kupata matokeo mwanzo na kushinda kuyalinda ni maumivu kwa mashabiki ila hakuna namna kwa kuwa imetokea ni lazima tukbaliane na hali.

Kufungwa mabao 2-1 haina maana kwamba ndio mwisho wa kushindana bado kuna karata mkononi cha msingi ni kuangalia namna gani tutapambana.

Pia wikiendi iliyopita timu ya wananchi ya Yanga ilikuwa na mchezo wa kirafiki uwanja wa taifa dhidi ya Coastal Union mchezo ambao ulivuta hisia za wengi ambao ni wapenda soka.

Tumeona kwa sasa kumeanza kuwa na mabadiliko kidogo hasa kwenye upande wa morali ya wachezaji kupambana kupata matokeo mwanzo mwisho jambo ambalo linaonyesha kwamba kuna kitu kipya kimeingia kwa wachezaji.

Ikumbukwe kuwa kwenye mchezo huo kipindi cha kwanza Yanga ilikuwa nyuma kwa bao moja ambalo beki wa Yanga Ally Mtoni wengi wanapenda kumuita Sonso alijifunga katika harakati za kuokoa mpira.

Mechi ya kirafiki imechezwa kwa ushindani mkubwa na kila timu ilionyesha kwamba sio dhaifu licha ya kwamba kila timu haikuwa na cha kupoteza kwenye mchezo huo zaidi ya kuongeza nguvu kwa ajili ya kusuka vikosi vyao.

Tumeona mabadiliko ya Yanga hasa katika mipango na umaliziaji wa hatari ambazo wanazitengeneza licha ya kuwa na makosa ya hapa na pale ambayo kwenye kila timu huwa hayakosekani na ni lazima yapatikane hasa kwenye mchezo wa mpira.

Kwa sasa timu inacheza inapata matokeo tena katika wakati ambao hakuna shabiki anatarajia jambo ambalo linamaanisha kwamba kwenye soka kila kitu kinawezekana kikubwa kujituma na kupambana kutafuta matokeo chanya.

Mwanzo mzuri kwa sasa kwa timu ya Yanga ikiwa chini ya kocha Boniface Mkwasa ambaye ameanza vema na timu yake akiwa ni kaimu baada ya kupokea mikoba ya kocha Mwinyi Zahera ambaye ameshatimka kwa sasa ndani ya Yanga.

Kuna muunganiko mzuri ambao upo kwa sasa ndani ya Yanga kila mchezaji anaonyesha kile ambacho anacho kwenye miguu yake na anatumia akili kupambana  pamoja na nguvu mwanzo mwisho bila kujali aina ya matokeo ambayo wameyapata.

Kwa kushindwa kuwa kwenye mwelekeo mzuri mwanzo kwa sasa ni hatua nyingine ya kubadili upepo ndani ya Yanga kuanzia benchi la ufundi pamoja na wachezaji kiujumla.

Wao wanapaswa waangalie walipokosea awali ili watengeneze matokeo chanya na mpango kazi makini ambao utawapa mwanga wa kupata mabadiliko tofauti na mwanzo namna iliyokuwa.

Wamepata mabao mengi kwenye mchezo wa kirafiki ambao uliisha kwa Yanga kushinda kwa mabao 3-1 jambo ambalo kwa kiasi fulani limerudisha morali kwa wachezaji na kuwapa nguvu mashabiki.

Timu inacheza mpira uwanjani na mbinu mpya zinaonekana kila mchezaji hayupo tayari kuona anapoteza nafasi ambazo wanazipata licha ya kukosea muda mwingine.

Wachezaji wanapambana ile ari ya wachezaji kwa sasa inaonekana hii ni hatua ambayo inapaswa ipongewe na wachezaji waongeze juhudi kwani kazi bado ipo kwa sasa.

Hivi vinavyoonekana kwa sasa vilikuwa vinakosekana awali kwa wachezaji na mashabiki walikuwa wanahitaji kuona namna gani wachezaji wanapambana kupata matokeo wakati ambao wanahitaji matokeo ndani ya uwanja.

Licha ya kupoteza mchezo mmoja wa kirafiki mkoani Mtwara kwa kufungwa bao 1-0 ni dhahiri kwamba kuna kitu ambacho walikipata walipopoteza na sasa wamezinduka rasmi.

Wengi walikuwa wachezaji wa timu b kwenye timu iliyofungwa mkoani Mtwara na kwa sasa ni suala la kutazama wapi walikosea na kuanza kuunda upya timu ambayo itakuwa na ushindani ndani ya ligi.

Licha ya ukweli kwamba wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza waliukosa mchezo wa pili mkoani Mtwara Ila kwa kuwa wengi wa kikosi cha kwanza walipumzishwa ni wakati muafaka wa kuona kwamba waliopumzishwa wamefanya kweli mchezo wao wa tatu.

Wanachama wanavutiwa na wameanza kuona matokeo ndani ya uwanja jambo ambalo litaongeza umakini kwao kujitokeza kwa wingi ndani ya uwanja na itaongeza mvuto kwa mashabiki.



3 COMMENTS:

  1. kama unaandika hbr za Timu ya Taifa zungumzia timu ya taifa usichanganye na hbr za Yanga

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ukisikia "niletee pilau makande" ndo hii

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic