November 22, 2019


LIGI Kuu Tanzania Bara ilisimama kwa muda kutokana na michuano ya timu za Taifa ambazo zilicheza mechi zao za kimataifa ambazo zipo kwenye kalenda ya Fifa.

Kwa kuwa nasi pia timu yetu ya taifa imekuwa na majukumu ya kitaifa ni mwanzo mzuri kwa mashabiki kuendelea kuiombea timu kuendelea kupata matokeo chanya kwenye mechi ambazo zimebaki ndani ya michuano ya kimataifa.

Mashabiki na taifa kiujumla limeshuhudia mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa taifa na Stars ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 jambo zuri na linapaswa pongezi kwa wachezaji kujituma bila kusahau mashabiki ambao wamekuwa bega kwa bega na timu ya taifa.

Kujitokeza kwenu kwa wingi uwanja wa taifa ni uzalendo tosha na inaonyesha namna gani mnapenda timu yenu ifanye vema kwenye michuano ya kimataifa na zile mechi za kirafiki.

Moyo huo unapaswa uendelee siku zote bila kuchoka inaonyesha ni namna gani tumekuwa wazalendo na tunajali kile cha kwetu ambacho tunacho hasa timu ya taifa ambayo ni ya kila mmoja.

Hakuna ambaye anapaswa kusema kwamba hastahili kuishangilia timu ya taifa kwenye kazi ya taifa ambayo ni mwanzo wa safari kuelekea kwenye michuano ya Afcon inayotarajiwa kufanyika 2021 nchini Cameroon.

Mchezo uliopigwa nchini Tunisia ni mwendelezo wa kuelekea kwenye mafanikio na ushindani upo kwenye mechi zote kwani kazi ya kwanza iliisha vizuri uwanja wa taifa kazi ya pili ilikuwa ngumu kidogo.

Kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1 haijawa furaha kwa mashabiki pamoja na wachezaji kwa kuwa imetokea ni sehemu ya moira na kujifunza zaidi.

Hakuna kukata tamaa kwa wachezaji wote wa timu ya taifa na benchi la ufundi bila kujali aina ya matokeo ambayo wanayapata ni mpira.

Kazi ambayo inapaswa iendelee kwenye maisha ya soka ni kuangalia ni namna gani timu itapata matokeo na itasonga mbele kwenye mechi zilizobaki ukizingatia kwamba kila timu ina mechi nyingine mkononi.

Wito wangu kwa mashabiki wasiisahau timu ya taifa kwenye dua zao wasiishau na timu ya taifa ili hali inaendelea na safari pamoja na maisha ambayo yapo kila siku katika soka.

Kikubwa ambacho tunapaswa tukifanye kwa sasa ni kuona kwamba kila mmoja anapenda kuona timu yetu inazidi kuwa na nguvu bila kujali aina ya matokeo ambayo wanayapata uwanjani.

Ni wakati mwingine wa kuendelea ile kampeni ya kusaka tiketi ya kuelekea kwenye mafanikio ya taifa letu kwani kushinda kwa timu ni mafanikio yetu sote.

Umoja ni nguvu na kila mmoja anapaswa asikate tamaa muda bado upo na kila kitu kinawezekana kwenye soka ni suala la muda na kila mtanzania aendeleze uzalendo kwenye timu yake ya taifa.

Wachezaji wa Stars jukumu lenu ni moja tu uwanjani kutafuta matokeo bila kukatishwa tamaa hata pale ambapo mnashindwa kupata matokeo ambayo mlikuwa mnafikiria kuyafanya.

Muda siku zote si jambo la kusubiri kwani ukibaki nyuma unaachwa jumlajumla katika kazi zako ambazo unazifanya napenda kuona kila mmoja anatimiza wajibu wake.

Kwa namna ambavyo watanzania wanawaamini basi nanyi kwenye mechi zenu nyingine mnapaswa mpambane kutafuta matokeo mkiwa uwanjani kwa kupambana mwanzo mwisho.

Kwa upande wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) tunaona bado linapambana kuona timu zetu zote zinapata mafanikio ambapo kwa sasa kuna michuano ya Cecafa kwa upande wa Wanawake.

Mashabiki hili pia ni letu watazania tujitokeze kwa wingi kuwapa sapoti akina dada wa Kili Queens ili wabebe kombe lao lingine la tatu litakalobaki jumla hapa Bongo.

Hicho ndicho ambacho mashabiki na watanzania tunahitaji kukiona hapa kwenye ardhi ya Bongo.
Kila mchezaji atambue kwamba jukumu lao uwanjani ni kutafuta matokeo na kufanya vile ambavyo wanaelekezwa na viongozi wao kwani kila kitu kinawezekana.

Zanzibar imeanza kwa kusuasua kwani haijapata ushindi kwenye mechi zake tatu na kocha wao amesema kwamba tatizo hilo ameliona na atalifanyia kazi.

Kufungwa haina maana kwamba hawana uwezo bali ni makosa ambayo wanayafanya kushindwa kufanyiwa kazi nina amini wakati ujao wakijipanga watakuwa na matokeo chanya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic