November 20, 2019


Baada ya kuzagaa taarifa mbalimbali mitandaoni kuwa huenda akawa amefutwa kazi kunako kikosi cha Simba, Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems anatarajiwa kutua leo jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Simba zinasema Aussems alielekea kwao Ubelgiji kwa ajili ya matatizo kadhaa ya kifamilia na inaelezwa atarejea leo nchini.

Kocha huyo ameibuka na kusema alienda kwao kwa ajili ya majukumu ya kifamilia na atarejea kuendelea na kazi kama kawaida kuelekea mechi ijayo ya ligi dhidi ya Ruvu Shooting.

"Niliondoka Tanzania kuelekea nyumbani kwa siku mbili, ninatarajia kurejea Tanzania leo kuendelea na majuku ya kuiandaa timu kuelekea mechi ijayo dhidi ya Ruvu Shooting," alisema Aussems.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic