November 19, 2019


KIBARUA cha Kocha Mkuu wa Tottenham Hotspur, Mauricio Pochettino kimeshikiliwa na mabosi wake kabla ya kuamua ni lini na siku gani watamfungashia virago vyake ndani ya timu hiyo inayoshirkik Ligi Kuu England.
Habari za ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa, mabosi wa Spurs hawajaridhishwa na uwezo wa kocha huyo msimu huu kutokana na kushindwa kuwapa kile ambacho walikitarajia awali ndani ya timu hiyo.
Spurs kwa sasa ipo nafasi ya 14 kwenye ligi kuu ikiwa imejikusanyia pointi 20 ikiachwa kwa pointi 20 na vinara wa ligi ambao ni Liverpool wenye pointi 34, baada ya kuchezwa mechi 12.
Inaelezwa kuwa Spurs inawapigia hesabu Eddie Howe, Julian Nagelsmann na Carlo Ancelotti ili wakatwae mikoba ya Pochettino.
Spurs imepoteza juma ya mechi nne na imelazimisha sare tano huku ikishinda mechi tatu pekee jambo ambalo limewapa wasiwasi mabosi wa timu hiyo kuhusu mwenendo wa kocha huyo wakihofia timu kushuka daraja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic