November 18, 2019

SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania amesema kuwa licha ya hali ya hewa ya nchini Tunisia kuwa tofauti kidogo na Tanzania watajua cha kuwafanya kesho uwanjani wapinzani wao Libya.
Tanzania itashuka uwanjani kesho kucheza mchezo wake wa pili kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya Afcon nchini Cameroon 2021.
Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema kuwa wachezaji wana morali kubwa na wanajua walichotumwa na watanzania hivyo hali ya hewa kwao si tatizo kupata matokeo chanya.
“Hali ya hewa ya huku ni tofauti kidogo na Tanzania ila haitufanyi kwamba tuwe na presha kazi yetu tutaifanya uwanjani na kumalizana nao wapinzani wetu, watanzania wazidi kutuombea ili tufanye vema.

“Unajua wachezaji wetu wamekuwa na juhudi na wanatambua kazi kubwa ni kutafuta ushindi, licha ya kushinda mbele ya Equatorial Guinea tulichelewa kuwafunga kwani kazi ilibidi iishe kipindi cha kwanza hivyo ni somo kwetu tumejifunza,” alisema Matola.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic