November 18, 2019


MABAO matatu aliyoyafunga mshambuliaji wa Azam FC, Kassim Suleman kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Friends Rangers uliochezwa uwanja wa Chamazi juzi umekosha Kocha Mkuu Arstica Cioaba raia wa Romania.
Azam FC ambayo inajiandaa na mchezo wake wa ligi dhidi ya Mbao FC utakaopigwa Novemba 23 uwanja wa CCM Kirumba ilishinda kwa mabao 6-0 jambo lililoongeza morali ya timu kuelekea mchezo wao huo.
Akizungumza na Saleh Jembe,  Kassim alisema kuwa mabao yake matatu yamempa nguvu ya kuendelea kupambana huku akipewa pongezi na mromania kwa kazi aliyofanya.
“Tunacheza tukiwa ni timu na kila mchezaji anahusika kwenye ushindi wetu, tunafurahi maisha yetu ya ushirikiano na kila mmoja anafurahia, kocha aliniambia kwamba ninapaswa kuongeza juhudi jambo ambalo linazidi kunipa mwanga wa mafanikio,” alisema Kassim.
Mabao mengine ya Azam FC yalifungwa na Mudhathiri Yahaya, Idd Kipagwile na Donald Ngoma, Azam FC ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 13 kwenye msimamo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic