JURGEN Klopp
Meneja wa Liverpool ana kibarua kizito Jumapili ya Novemba 10 uwanja wa Anfield
itakapomenyana na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England Manchester City ambao
ni wapinzani wao wa karibu kwa sasa ndani ya Ligi Kuu England.
Liverpool
itaingia uwanjani ikiwa haijaonja ladha ya kupoteza mchezo wa ligi baada ya
kucheza mechi 11 ikiwa imeshinda mechi 10 na ililazimisha sare moja ya
kufungana bao 1-1 mbele ya Manchester United kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa
Old Traford huku City ikiwa imepoteza mechi mbili, sare moja na imeshinda nane.
Manchester
City iliyo chini ya Pep Guardiola inaingia ikiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Southampton uliopigwa
uwanja wa Etihad huku Liverpool ikipindua meza kibabe mbele ya Aston Villa
ikiwa ugenini kwa ushindi wa mabao 2-1 uwanja wa Villa Park.
Liverpool
ipo nafasi ya kwanza imejikusanyia jumla ya pointi 31 huku City ipo nafasi ya
pili ina jumla ya pointi 25, kwa upande wa Meneja wa Liverpool Klopp amesema
kuwa anatambua mchezo utakuwa mgumu ila watapambana kupata matokeo huku
Guardiola Meneja wa City amesema kuwa watafanya kazi kubwa kutafuta ushindi
ugenini.
0 COMMENTS:
Post a Comment