BONIFACE Mkwasa, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa siri kubwa ya ushindi wao mbele ya Ndanda jana ni juhudi za wachezaji wake kucheza kwa kufuata maelekezo bila kuchoka.
Ndanda FC ilipoteza mchezo wake ikiwa nyumbani kwa kufungwa bao 1-0 lililopachikwa na Patrick Sibomana dakika ya 75.
Mkwasa amesema kuwa kwa sasa kikosi bado hakijatengamaa vema kutokana na kuwakosa wachezaji wake muhimu ila ana imani kitarejea kwenye ubora.
"Tunaanza kutengamaa kwani wachezaji wana morali kubwa ya kufanya kazi na kujituma katika kile wanachokifanya ni muda wa mashabiki kuendelea kutupa sapoti.
"Ushindi wetu umetokana na juhudi za wachezaji kucheza kwa kujituma na kufanya kazi ambayo imewapeleka uwanjani," amesema.
Ushindi wa jana umewafanya Yanga kufikisha jumla ya pointi 10 ikiwa imecheza mechi tano mpaka sasa za Ligi Kuu Bara.
0 COMMENTS:
Post a Comment