UNAI Emery kocha wa Arsenal nafasi yake ndani ya kikosi cha Arsenal inazidi kuwa finyu baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Eintracht Frankfurt ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Emirates.
Licha ya kipindi cha kwanza Arsenal kuongoza kwa bao moja lililofungwa na nahodha Pierre Aubameyang mambo yalibadilika kipindi cha pili ambapo Daichi Kamada alipindua meza kibabe kwa kufunga mabao mawili na kuifanya Arsenal kupoteza mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mchezo wa mwisho kwa Unai Emery kushinda ilikuwa ni Octoba 24 mbele ya Vitoria SC uliokuwa ni wa Ligi ya Mabingwa akishinda mabao 3-2 kwenye mechi zake zote za mwezi Novemba hajaonja ushindi kwenye jumla ya mechi tano alizocheza mpaka sasa.
Alilazimisha sare mechi tatu na kupoteza mechi mbili jambo ambalo limewakasirisha mashabiki wa Arsenal wakihitaji kumuona kocha huyo akisepa mazima.
0 COMMENTS:
Post a Comment