Kiungo wa Simba, Sharaf Shiboub ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Sudan.
Shiboub amejumishwa katika kikosi hicho ambacho kitacheza michezo miwili ya kufuzu AFCON 2021 dhidi ya Sao Tome (13 / Novemba) na Afrika Kusini (17 / Novemba).
Wakati Shiboub akisafiri kuelekea Sudan kwa ajili ya kibarua hicho, hapa Tanzania, Kocha Mkuu wa Taifa Stars ametangaza kikosi kwa ajili ya mechi za kufuzu AFCON pia dhidi ya Libya na Guinea.
Katika orodha hiyo, jumla ya wachezaji saba wa Simba wameitwa katika kikosi hicho ambacho ni ambao ni Mohamed Hussein, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Miraji Athumani na Hassan Dilunga
0 COMMENTS:
Post a Comment