JAMIE Vardy nyota wa Leicester City ni kinara wa kucheka na nyavu ndani ya Premier League kwa sasa akiwaacha kwa mbali waliotwaa tuzo ya kiatu bora msimu uliopita.
Amecheza jumla ya dakika 990 anafunga bao moja kwa wastani kila baada ya dakika 99 akiwa ndani ya Uwanja.
Amefunga jumla ya mabao 10 mpaka sasa na ametoa Asisti moja tu ya bao.
Kwa waliotwaa tuzo ya kiatu msimu uliopita anayefuata ni Aubameyang mwenyewe ametupia mabao 8 hana asisti, Sadio Mane ametupia 6 akiwa na asisti mbili na Salah ametupia mabao matano na ana asisti tatu.
Nyota hawa walitwaa kiatu cha dhahabu baada ya kugongana kwa upande wa kutupia msimu wa 2018/19 wote walitupia jumla ya mabao 22.
Page zako ukibadilisha kuzisoma kwa kiingereza hazileti maana iliyokusudiwa karibu kurekebisha
ReplyDelete