Imeelezwa kuwa Kaimu Kocha wa Yanga, Boniface Mkwasa amesema hivi sasa analenga kufanya usajili wa straika wa maana ili kukiboresha kikosi chake.
Taarifa za ndani zinasema Mkwasa amedai kuwa mpaka sasa kumekuwa na mapungufu katika safu ya mbele japo ambalo linasababisha kusiwe na mabao mengi.
Mkwasa ameeleza Yanga imekuwa ikijitahidi kushambulia lakini kumekuwa hakuna matunda na hata muunganiko wa mbele bado unaleta utata.
Amezidi kufunguka kwa kusema lengo lake ni kuona mabosi wake wanakubali kutoka fedha ya usajili ili aletewe mshambuliaji mwenye bidii atakayewapa changamoto wapinzani ili kucheka na nyavu.
“Ukiangalia timu ina washambuliaji wazuri lakini tunamkosa
mtu anayeweza kufunga. Yaani mtu akipata nafasi anaitumia
kwa kufunga…sio yule anayepata nafasi tano kisha anafunga
moja. Tunatengeneza nafasi nyingi hata mazoezini na
washambuliaji wanafunga, lakini nataka iwe zaidi kwenye
mechi.
“Nitakutana na viongozi wangu na kuwapa mapendekezo
kuhusu nini cha kufanya kwenye dirisha dogo la usajili. Lakini,
kubwa nataka mshambuliaji mwenye uwezo wa kufunga.
Natambua wako wengi lakini, ni suala la kukubaliana ni nani
tutamchukua iwe kutoka hapa ndani ama nje ya nchi lakini hadi
tukubaliane na uongozi,” amesema Mkwasa
Masikini hana kiapo we mkwasa unafukuzwa unazaririshwa bado unarudishwa tena kweli MASIKINI HANA KIAPO
ReplyDeleteVizur
ReplyDelete