November 8, 2019



NAMUNGO FC iliyo chini ya Hitimana Thiery imewaongezea machungu Ruvu Shooting ya kupapaswa mabao 2-0 na Ndanda FC kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona kwa kuitungua mabao 2-1 mchezo uliopigwa Uwanja wa Majaliwa.

Ushindi huo unaifanya Ruvu Shooting kuacha jumla ya pointi sita zote mkoani Mtwara na kubebeshwa zigo la mabao manne huku wao wakiambulia bao moja tu.

Akizungumza na Saleh Jembe, Thierry amesema kuwa wachezaji wake wanajua wanachotakiwa kufanya wakiwa uwanja wao wa nyumbani Kwa kuwapa raha mashabiki ili kujiongezea hali ya kujiamini.

"Tumekuwa tukipata shida tukitoka hapa Majaliwa kutokana na wachezaji wangu kushindwa kujiamini ila kwa sasa kuna kitu ambacho ninakijenga tutakuwa sawa, kikubwa sapoti," amesema Thierry.

1 COMMENTS:

  1. Uchambuzi mzuri, lkn umetiwa dosari na aya ya pili inayosema Ruvu Shooting imeacha pointi sita mkoani Mtwara. Ukweli ni kwamba, Ndanda na Namungo ni timu zinazotoka mikoa miwili tofauti, Ndanda ya Mtwwara na Namungo ya Lindi. Naomba kuwasilisha.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic